Jumapili, 3 Januari 2016

SIKITIKO LANGU (siku uumbiwa shida)






Mwili wake uliojengeka kikamilifu,kifua kipana na urefu wake uliosindikizwa na ngozi ya maji ya kunde vilimshawishi kila binti kukiri kwamba Eze kado alikuwa mtu wa shughuli pevu kitandani,"Umbo langu halijengwi na mpira wa miguu wala gym" alipenda kujitapa Eze kila anaposifiwa kwamba "He is gentleman" ni ukweli mtupu wala alikuwa hajisifii hata kiduchu Japo maisha yake yalikuwa ya kawaida sana hakuwa na makuu ila sifa zake zili enea zaidi kutokana na maneno ya majirani zake hasa wasichana walikwisha kuonja mambo yake.
Kutoka na maisha duni ya vijana wengi walio kuwa katika mtaa mmoja hasa wale waliokuwa  na urafiki pamoja na Eze waliona mambo anayofanya ni kama laana Kitendo cha mtoto wa kiume kuwa tayari kufanya mapenzi kwa ajili ya pesa lilikuwa jambo la ajabu sana kwao na sio ivo tu kwani jambo hili na vitu vilivyokuwa vinafanyika na Eze vilikuwa vitu vigeni katika macho yao japo Fikra zao na Mitazamo yao hata haikuwa na tija yoyote  kwa Eze yeye aliona swala hilo ni sawa tu tena ni ajira tosha na kama alipata nafasi ya kulitenda basi alifanya kwa juhudi zote na hii ni sababu tosha ya yeye kuweza kunasa warembo wengi tena wenye pesa zao.
Baadhi ya vijana waliokuwa na mtazamo tofauti na jinsi yeye alivyokuwa walikuwa akijitenga nae ili halikuwa tatizo kwake maana yeye Eze alikuwa mtu wa watu alipata marafiki wa kila rika kwani alikuwa mchangamfu,mcheshi na mwenye kusikia kama ataona jambo hilo kuwa zuri maisha yake yote yalikuwa ni ya kukutana na watu wapya na kufanya urafiki  kwa wale waliokuwa  wakiishi kwa wazazi wao daima hakupewa  ridha hata kidogo wazazi wao hakuwa wakipenda kuona vijana wao wakimbatana na Eze maranyingi waliwaambia wa mkwepe sana kwani wengi walikuwa na mtazamo sawa na falsafa hii UKIWA KARIBU NA UARIDI BASI NAWE UTANUKIA .
*****************************************************************************
Eze aliependa kuishi vile amabavyo akili yake ilikuwa inamtuma na hakuiona ubaya wala tatizo katika maisha ambayo yeye alikuwa ameichagua kuishi ,alipenda sana kuwa na marafiki wengi lakini kutokana na namna wengi wao walivyokuwa wanamchukulia kamwe hakuwa mtu wakisirani aliheshimu maamuzi yao na hata siku moja hakuwahi kuwa na Fikra ya kupata matatizo nje ya lile la kufumaniwa akiwa na mke wa mtu maana alijua fika mambo yatakayo mkumba siku iyo atakayo fumwa hofu iyo ilifanya akawa muoga sana kufuatilia au  kuwa karibu na wake za watu hakupenda kabisa mazoea nao.
Katika mawazo yake sio kwamba alikuwa hana tamaa kwa hawa wake za watu laa woga wake tu ndo ulifanya atafute njia ya kumuepusha yeye juu ya mabalaa yatakayo mpata pale atakapo fumwa na mke wa mtu aliweza kujikinga kiasi chake na akili mwake alikuwa na kauli moja tu ya kumlinda  katika  swala hili kwamba MKE WA MTU NI SUMU.
Eze alikuwa mtu wa totoz  kila wiki aliweza kubadili hata mara tatu,si yeye aliyewatongoza mara nyingi wengne walitaka huduma wenyewe hata bila ya yeye kutamka Neno "NAKUPENDA"kati yao,mh! sijui walikuwa wanapata nini lakin kamwe hawakuisha wala kukatika katka ghetto la Eze hakuwa na kazi maalum lakin kutokana na kujibanabana kwake aliweza kupanga chumba katika nyumba ya Mzeejobu mahali ambapo palikuwa kipozeo cha walimbende wengi na walikuwa wana kuja na visingizio vingi vingi tu mara watake chaja ya simu,wengine walikuwa wanakuja kulizia muda katika ghetto lake hakuwa na mambo mengi sana ,maana lilikuwa ni ghetto la kisela zaid yeye alikuwa na kitanda ,redio,kijimeza kidogo kilichokuwa na kopo la kuwekea mswaki/dawa na vitu vingne vidogovidogo tu  ila ukifika muda wao tu wenyewe walikuwa wanakuja ili mladi tu kumuona au kusikia sauti yake.
Kitanda chake ni rafiki zake pekee waliokiita sita kwa sita lakin kila binti aliyebahatika kulala
chali au walau mikono tu ndo kushika kitandani wakat miguu iko chini walitoka na majina yao
tofauti,wengne walisema 'konani ' wengne 'darajani' na wengi wao walipaita "MACHINJIONI" jina la MACHINJIONI hili ndo lilikuwa maarufu sana kwa wote waliokuwa wanaishi na Eze katika nyumba ile haswa wale waliojua tabia yake wengi walikifanisha  chumba chake na #Boma yaani (sehemu ya kuogeshea mifugo kila ngo'mbe,mbuzi,kondoo wa kila aina  lazima azamie kwenye maji yake haijalishi mnyama huyu atakuwa na afya njema au mgonjwa) ni lazima hataoshwa tu, ivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Eze kamwe hakuchangua msichana wakulala nae awe mweusi ,mweupe ,mnene,mwembamba au MSICHANA mwenye sifa yoyote aliochozingatia yeye ni uzima wa afya zao tu japo hakuwa tayari hata siku moja kwenda kujipima gonjwa lolote la zinaa.
Maisha haya kwake Eze yalikuwa mazuri tu na alifurahia sana kwa namna moja yaliweza kuraisisha ugumu katika swala la uchumi kwani  katika siku zote yeye hakuwa mtu wa presha kwamba sina hela ,chakula au mavazi kwani baadhi ya wasichana wengi aliokuwa nao walikuwa wakijiweza kiuchumi na pale walipo kuwa wamefuraishwa au kukunwa ile inavyopaswa  waliweza kukunjua  pochi zao kwa rohosafi kabisa na kumkabizi kiasi kidogo cha pesa cha kusaidia katika mahitaji yake pale.
Eze hakuwa na kumbukumbu ya kulalamikiwa na msichana eti kuwa hajaridhika hata kama siku iyo alikuwa na uchovu kasi gani yeye alifanya kila njia kuweza kufuraisha moyo wa binti yoyote atakaye kuwa nae kwa wakati huo badala yake weng walimwambia "Eze unaniua" wakati kiuno bado wanazungusha.ah! mapenzi bwana mambo haya yalikuwa yakimfuraisha sana Eze na alikuwa najiona kidume haswa
Kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi wa wapangaji ambayo alikuwa anaishi nao katika nyumba ya Mzee jobu alilazimika kuhama na kwenda katika mtaa wa mbali kidogo  na hapo alipokuwa akiishi mwanzo sababu kubwa ya kufanya yeye kuondoka ni baada mmoja wa wapangaji wenzake aitwae baba sukudhan kuhisi kuwa Eze anatembea na mkewe kwa woga alikuwa nao Eze hakupenda mambo kuwa makubwa sana na njia peke akaona ni bora kuondoka tu mahala pale kwani tabia yake ilikuwa nongwa kwa wapangaji wenzake hasa wale wote waliokuwa na wake zao.

Pamoja na kuponapona toka katika lawama na mtego wa babasikudhan hakuwa mwisho wa tabia ya Eze japo swala hili lilikuwa nyenzo tosha ya kumfanya yeye kuwa makini zaidi kwa ugeni wake pale mtaani wengi hawakuwa na mazoea na tabia yake japo walikuwa wanajua sifa zake chache tu .