Yahaya; Ndugu yangu najua wajua fika kuwa wiki kadhaa
tu koo yangu ilipatwa na tatizo na kuondokewa na mmoja wa ndugu muhimu sana ndio nalijua hilo si kuhusu kufariki kwa
Bwana Matango {kudu alidakia} haswa
sasa na ndhani wakumbuka kuwa adhima yangu ni kuwa na mimliki kubwa na nzuri na
pahala pa kufanikisha hili ni katika kushika milki ya huyu ndugu yangu na swala
hili litatukia baada ya wiki ya pili ya msiba kwisha yaani siku ya kuanua
matanga wote tutakapokuwa kwenye kikao
cha wazee wa koo shida ni kwamba taratibu za koo hazinipi ruhusa ya kushika
mali hizi rafiki yangu naomba busara zako kwani kichwa changu kina chemka.
Kudu;mhh sasa hapo mie sidhani kama nitakuwa na uwezo
wakufanza lolote maana kuna mambo ambayo unataka kuchanganya na mwisho wake
uwaga sio mzuri kakangu
Yahaya; kwanini ushindwe na mambo gani hayo unayoyaongelea wewe?
Kudu;Unajua vitu tunavyofanya sikuzote uwa ni mabaya
ila kwakuwa tunafanya kwa maslai binafsi uwa tunafanya kuwa halali ila katika
swala hili na maelezo yako hayo hapo kuna busara
za wazee na tambua fika maamuzi yao uwa hayapingwi kwakuwa wanatumia hekima
zao pili kuna mila na desturi katika
jambo hili hata kama nitakupa mashauri ukumbuke hii miiko iliyopo kwenye jamii
yetu haswa katika jambo hili ulilokujanalo.
Yahaya;Sawa hayo yote nayatambua vyema lakini namie
nina matamanio yangu na ndio sababu ya kukutafuta na kukuleta mpaka pahali hapa
nakutambua vyema bwanaKudu na nina imani kuwa hata wewe wanitambua vilivyo na
hali zangu wazijua fika sina hakika kuwa
utaniona lofa au kuniweka katika kundi la wapuuzi kwa maamuzi haya niliyonayo
Kudu;kwasasa saivi ndo naelewa adhima yako vilivyo na
naomba ukumbuke mambo mawili yale niliyosema ukisha kubaliana nayo hapo nami
nitakuwa na nafasi ya kueleza maono yangu ili tusiweze kulumbana sana nakubaliana nayo {ilikuwa sauti ya
kinyonge toka kwa Yahaya} hapo sawa sasa jambo la kwanza ilikuweza kushawishi
hisia na busara za wazee pamoja na mamaChiku mwenyewe badili msimamo wako uwe
chanya kwa watu wote hawa
kohkohhkohoKudu
alitoa kikohozi cha kusafisha koo lake iliaweze kusikika vyema kisha akaendelea
kama utafanya shingo yako kuwa ngumu katika hili tambua fika mawazo ya wazee
yatakuwa kinyume na wewe na tena katika mila na desturi za hapa linapotokea
swala kama hili wazee wanaangalia hali ya familia husika na kama mama wa
familia anajiweza wao umpatia jukumu la kutafuta mtu wa kumrithi na
kummilikisha mali zote binafsi yangu naona hii ni nafasi pekee ya kumshawishi
mamachiku kukubaliana na matakwa japo sio kwaku mueleza yale utakayo laa ila
jaribu kuteka ule ukaribu wako kwake sijui kama tu pamoja.
Yahaya;mmmh mh haya maji ya shingo ila hakuna tatizo
ngoja nitaona itakavyokuwa kabla ya siku kufika
Maono
ya yahaya sasa yalikuwa yakiwaza utajili wa mali kedekede na kupewa mtu wa
kupokea kauli na maagizo yake bila kuhoji nini cha ziada moyoni mwake hakuwa na
lepe la huruma kwa familia hii iliyojawa majonzi
Kudu;ndugu yangu swala lolote linanalo hitaji mikono
na busara za wazee uwa sio jambo jepesi lakini nadhani itafaa kama ukimrithi na
mfiwa mwenyewe
Yahaya;mmh eeenh hapo hapa tena ilo swala hata
silitaki kabisaa…yani pale mie nataka mali tu maisha ya chiku na mamaye sitaki
yawe yangu hata punje.
Kudu;basi hapo ndo unapokosea ila hakuna namna na mie
mpaka sasa sina la kuongeza kama kila neno unaona mzigo hapo namie na nanawa
mikono kaka tusubiri maamuzi ya balaza la wazee hatuna uwezo wa kuingilia
watakachotaka kufanya.
Yahaya;mwee sawa rafiki yangu katika hili nimeingia
mkenge ila katika ukoo wote mie ndo mkubwa na hili swala hakika litakuja kwangu
tu.
Kudu;sawa tusubiri ….. af wakati unatuacha ebu tuanze
kurejea
Wakati
haukuwa rafiki kwao ilibidi wanyanyuke nakuanza kujerea majengo Yahaya
hakuamini kama swala hili limekuwa gumu kiasi kwamba hata kudu alikuwa na nafsi
ya uwoga kutoa na kueleza mashauri yake juu ya namna ya kulifanikisha na njia
nzima bado alikuwa akiona giza kubwa kwani hakuona hatma ya kile alichokuwa
akitaka kupata.
Akiwa katika chumba chake Kapemba bado alikuwa na
taswira nzito kwa kujaribu kutengeneza picha ya namna ambavyo kijana wa umri
wake anavyokutana na changamoto nzito na kukosa msaada wa kuzitatua,alijaribu
kufikiria hali ya maisha katika kijiji chao ilivyokuwa hapo awali na kulinganisha na
hali aliyoipata katika sauti ya Sada katika siku ile marazote alipotaka kupata
usingizi sauti na sura ya huzuni iliyokata tamaa ya rafikiye kipenzi sada
ilijitokeza na kufanya usingizi kuwa wenye maruweruwe mengi hapana nitasema na Baba kesho labda atakuwa
anajua chanzo {alijisemea Kapemba na kulazimisha kujilaza}
Usikose kufuatiali sehemu ijayo..............
