Jumatatu, 31 Agosti 2015

SAFARI YA ISOKE

ILIPOISHIA 

Siku Zote nilijibidisha kuwa mfano bora ili niweze kupata mchumba, nilikuwa mtiifu, nikiwa heshimu wenzangu na kushirikiana nao vema kujenga Taifa.Kujaribu kuwa na marafiki wengi wa jinsia tofauti.

ENDELEA 


Nilijitahidi nikihisi pengine wale marafiki wangenifaa kumbahatisha wa ubani wangu.
Pamoja na yote hayo sikuweza kubahatika kupata niliyempenda kutoka moyoni, na aliye ni penda, Nilizidi kumuomba Mungu anishushie neema ya kumpata wa ubani wangu.

Ikafikia wakati nikaomba ushauri, lakini wale niliowaomba ushauri walionekana kuwa fukara wa mawazo, Walinishauri wakisema kuoa ni kuoa.Eti mwanamke ningemfunza mimi mwenyewe kama atakuwa na tabia mbaya.

Nikafikiri mara mia mia ushauri wao nikaona haukuwa na maana zaidi ya upofu.“Bw #kagoma inamaana uwingi wa wanawake ulimwenguni umekosa umpendaye?” Lilikuwa swali nililoulizwa na rafiki yangu katalambuga .Hatahivyo nilishndwa  kumjibu na hatimaye nikamdharau.“Inamaana kuchagua mke wa kuishinae ni kosa????, pengine ni kama kupewa mtihani wa somo usilo jua na kusubiri matokeo mazuri??? au hili swala ni sawa na kuokota fungu la samaki sokoni ama vipi?”Nilijiuliza Maswali mengi bila kujijibu kwa wakati huo.

Itaendelea tena

SAFARI YA ISOKE

Sehemu ya Kwanza


MTUNZI ; Kado¦Kadidi 

                                                   

Nilikuwa nikifanya kazi katika kampuni moja ya usafirishaji wa madini hapa hapa nyumbani Tanzania na wakati fulani nilikuwa natoka njee ya mipaka ya Tanzania kupeleka madini nchi kama  Bang kok nchini Thailand n.k Kampuni yetu ikiwa ya mtu binafsi na ilikuwa wilayani  SIKONGE katika mkoa wa TABORA .

Mimi ni #kagomaKapaku ndiye niliyekuwa idara ya usafirishaji, nikiwa afisa mauzo. Katika maisha yangu yote nilitegemea sana na nilihitaji kuwa na mwenzi wa kuishi naye, kama
vile familia nyingine bora ambazo kila siku zina furaha na ridhaa.Kwa kila mmoja kuwa
mwanandani wa mwenzake. 

Pia nilikuwa namuomba Mungu kwa kila hali si kanisani na hata nikiwa katika mapumziko yangu, anipatie mwanamke ambaye angenifaa katika maisha yangu.Kila siku palipokucha,niliamka nikiwa na wazo la kumpata nimpendaye na anipendaye.Niliamini hivyo japo sikuwa na uhakika kama kweli ningepata mtu kama huyo maishani mwangu.


Siku zote nilijibidisha kuwa mfano bora ili niweze kupata mchumba, nilikuwa mtiifu, nikiwa heshimu wenzangu na kushirikiana nao vema kujenga Taifa.Kujaribu kuwa na marafiki wengi wa jinsia tofauti. Nilijitahidi nikihisi pengine wale marafiki wangenifaa kumbahatisha wa ubani wangu.



itaendelea tena.....