Jumatano, 31 Agosti 2016

TAMU NA CHUNGU


sehemu ya pili



Kwao hakina chiku bado kulikuwa na songombingo la yahaya kutaka maamuzi ya wazee wa kaya ya mmpendekeze yeye kama ndiye mtu astahiliye kupewa mirathi japo kwa mujibu wa taratibu yahaya hakuwa mtu sahihhi anae faha kupewa miliki na mali za babake chiku alitambua fika kuwa kwa njia za kawaida hatoweza kuwashawishi wazee wale kukubaliana na mawazo yake pale itakapo wadia siku ya kuanua matanga,ikiwa ni jioni tulivu yenye upepo mwanana huku mida ikiwa inazidi yoyoma kuutafuta kigiza cha usiku aliona bora aende kilingeni kumtafuta rafikiye Kudu mawazoni mwake aliweka imani kuwa kutoka kwa rafiki yake huyu hatapata mawazo safi ya kufanya aweze kufanikisha mipango yake ya kupora na kumiliki  mali za MzeeMatango nyakati zote hawapo katika shuruba kudu ndiye aliyekuwa kimbilio lake na nyakati zote uwa asitikusilikiza mashauri anayopewa na rafikiye huyu moyoni mwake yahaya hakuwa hata na chembe ya huruma kwa hali watakayo kuwanayo wakina chiku pamoja na mamaye alichojali yeye ni kupewa miliki na kuzitumia mali hizi kwa namna itakayo konga nafsi yake vilivyo aliwaza anasa kuliko maisha ya upweke yatakayo anza kwa mama chiku na bintiye.

baada ya kufika kilingine alianza kupepesa macho kutafuta pahala alipoketi kudu 

ilichukua kama dakika mbili tu taswira ya kudu ilikuwa tayari katika mboni za macho yake mazoea ya kuwa wote kilingine yalimfanya yahaya asipate tabu sana kuzungusha mijicho yake ili kumpata rafikiye maana kudu alipendelea kukaa katika kona ya kati kalibu kabisa na kitijoto cha mamamuuza.

Nyakati zilikuwa zimesonga tangu alipoanza mwendo kwenda kilingeni jioni sasa nayo iliyoyoma na nuru ya jua ilianza kupoteza mwanagaza wake sababu ya usiri mzito wa mambo waliyotaka kuzungumza yahaya hakuona kama itakuwa busara kwa wao kuketi na kuendesha mazungumzo yao katika kilinge ila hakuwa na nguvu ya ushawishi kumuondosha kudu katika mazingira yale.

Yahaya; Habari ndugu yangu ,,,? Naona upo hapa kupumzisha akili kama ilivyo ada.
Kudu; aaahnahaha yahaya kijogoo cha mji mtu mwenye adhi yake ,, karibia sana kakamkubwa hapa si tupo tunaondoa mikosi na laana za wazee wa ardhi hii ya imarakaseko.
Yahaya; nakuona tu hapa maana upo na mashamshamu leo vipi mbona wale warembo wa pembeni hawapo pamoja nawe kunani? Umeanza yale mambo ya ajabu nisiyopenda (Kudu alilalama) basi tuachane na haya ndugu yangu mguu huu niwako nimekuja kukungata sikio ilikupata busara zako yahaya alisita kidogo
Kudu; endelea nakusikiliza mbona upo kimya tena ….! kama ni jambo la usiri sana tufanye kuzungumza baadae tukitoka hapa  au we wasemaje ?
Yahaya; rafiki yangu kama nilivyosema huu mguu ni wako na hapa sikuja kwa adhima nyingine yoyote ile zaidi ya kutaka kuonana nawe kuzungumza jambo hili basi,maana ili jambo lina ninyima raha na Amani ya kufanya mambo mengine hata kama nitajilazimisha vipi bado nakuwa sina uhuru kama awali napolifikiria swala hili sasa naomba tutoke hapa twende nje kidogo naitaji busara zako, mmmh kweli ili jambo la hatati sana mtu mzima mwenzangu mpaka umekuwa na hali ama kweli muungwana akivuliwa nguo sharti achutame haya twende huku njee {kudu alikubaliana na mawazo ya yahaya kisha wote wakanyanyuka na kuanza kwenda nje ya kilinge}
Kudu; haya mkubwa mwenzangu ebu ni habarishe kuhusu ilo swala maana ushaanza kutia ofu namie hapa naona nafsi inajawa mashaka Je kunani huku au lile sekeseke la wale wafugaji kutoka katika ardhi ya udongo mzuri limekuja tena?
Yahaya; hapana sio jambo hili walasindani kama lile swala la weza kurudi tena hili la leo ni jipya tena jipya haswa, skiliza ebu twende hapo kwenye mawe ya mtemi tukaketi hatuwezi kuongelea hili jambo hapa rafiki yangu
Kudu hakuwa na kinyonge wala hakutaka kubishabisha sana juu ya maombi ya yahaya japokuwa alitambua fika kuwa tayari raha zake zimekwisha katishwa na hatapata nafasi tena ya kuzirudia kwa wakati ule maana tayari nyakati zake zilikuwa zimekwisha muacha alifuatana na rafikiye mpaka katika sehemu ya mawe ya mtemi
Kudu; bwanamkubwa haya sasa tumefika ebu keti na unihabarishe juu ya hayo maswala yako nakuona hauko sawa na nadhani hata moyo wako pia una shuruba sawa na hali ya macho yako nipo hapa sema nami
Yahaya; Ndugu yangu najua wajua fika kuwa wiki kadhaa tu koo yangu ilipatwa na tatizo na kuondokewa na mmoja wa ndugu muhimu sana ndio nalijua hilo si kuhusu kufariki kwa Bwana Matango {kudu alidakia} haswa sasa na ndhani wakumbuka kuwa adhima yangu ni kuwa na mimliki kubwa na nzuri na pahala pa kufanikisha hili ni katika kushika milki ya huyu ndugu yangu na swala hili litatukia baada ya wiki ya pili ya msiba kwisha yaani siku ya kuanua matanga wote tutakapokuwa  kwenye kikao cha wazee wa koo shida ni kwamba taratibu za koo hazinipi ruhusa ya kushika mali hizi rafiki yangu naomba busara zako kwani kichwa change kina chemka.
Kudu;mhh sasa hapo mie sidhani kama nitakuwa na uwezo wakufanza lolote maana kuna mambo ambayo unataka kuchanganya na mwisho wake uwaga sio mzuri  kakangu
Yahaya; kwanini ushindwe na mambo gani hayo  unayoyaongelea wewe?

Usikose kufuatilia sehemu ijayo.

Jumamosi, 27 Agosti 2016

TAMU NA CHUNGU

utangulizi



Hapana kwa kweli kama hali itakuwa ivi siku zote hakuna hatakaye salia katika mjii huu kila kukicha hakuna nafuu wala afadhari leo unalala na hili kesho una aamka na lile mmh,hata kama ni umaskini hapa umezidi ama kuna anae tuchawi kwani hali hii sio bure Sada alikuwa akilalama mwenyewe pasipo kujua kuwa sauti yake ilisikika kwa Kapemba
Kapemba; Mwenzangu vipi mbona walalama pekeako uko utokako kuna heri..?
Sada; Mmh kama kungekuwa na heri wazani ningekuwa na hali .!!!! uko hapana afadhari wala unafuu
Kapemba; mapungufu uwa hayakosekani kwa binadamu ndugu yangu la muhimu ni kukubaliana na hali ilivyo tu kisha unatafuta njia ya kujikwamua hapo ulipokwama.
Sada; ama kwani we umwenyeji wa wapi..!!
Kapemba; mbona washituka..? mie ni mzawa wa hapahapa ila sipo hapa kwa kitambo kidogo
Sada; kumbe basi we ni wakuja na shida zetu sisi hapa bado ujazitambua vyema ukikutana na watu  kenda kama mimi nadhani utapata ufahamu japo kwa uchache na hauta shangaa tena kuona binti mdogo kama mie nikiwa katika hali ngumu kiasi cha kuchanganya kichwa change ivi.
Kapemba; samahani najua kila mtu anamahitaji na kupitia uhitaji wake hapo ndo changamoto zinapoanzia sasa mwenzangu naomba kwanza kufahamie kabla ya kufika mbali katika mazungumzo yetu mimi naitwa kapemba binti wa watatu wa Mzee Nsindano sijui waitwa nani?
Sada; eeh we ni binti wa Mzee Nsindano wa pale kwenye bonde la udongo mzuri Ndio hapohapo wala ujakosea {sauti ya Kapemba ilidakia} mwee kweli dunia duara na maisha yanabadilika kwakweli umekuwa rafiki yangu yaani kama vile babako alivyopataga bahati yakupata ardhi nzuri imekuiwa vivyo ivyo hadi na kwako Mmmh unasema nimebadilika kwani we nani na kilichobadilika ni kipi? {Kapemba alioji kwa sauti ya mshang`ao} ona sasa yani mpaka muda huu bado ujatambua waongea na nani sada alisema kwa kusononeka kisha akaendelea huko mjini sijui walikuwa wanakupa chakula gani ? kimekusahaulisha kila kitu cha huku  mimi ni malkia wa undazi.
Kapemba; aaahaaah jamani Sada Madoso masiku mengi yamepita rafiki yangu na mbona umekuwa ivi kulikoni tena pacha wangu maisha tu yamenichagua mwenzangu hakuna kingine {alidakia sada kwa sauti ya kinyonge iliyojawa simanzi} kapemba aliendelea Ebu nambie bhana kuna nini kimefanya uwe katika hali hii maana hata kama ni maisha kwa stahili hii uliyonayo hapana mwenzangu mtazamo wangu uwaga nyinyi saivi mtakuwa wafanyabiashara mashuhuri wa mazao ya hapa kijiji..
Sada; nadhani bado tupo pamoja nitakwambia tu na utaitambua hali halisi ya maisha yangu naya vijana wengine wa hapa kijiji nikianza kusema saiv haitakuwa vyema na waweza usielewe lolote kwani mabo haypo vile ufikiliavyo vijana wote wakipindi kile uwajuao hawapo tena
Sada alishindwa kujizuia nakuanza kulia kapemba alimsogeleana nakukumbatiana uku wote sura zao zikiwa na majonzi na macho yakiwa yanatirikwa na machozi ya simanzi yenye mchanganyiko wa furaha ya kukutana tena baada yakupotezana kwa kitambo kirefu ilikuwa yapata miaka takribani ishirini tangu kupotezana kwao taswira zao za utoto hazikuwa  zikionekana tena na wala zile fikra zao za kitoto juu ya maisha yao ya baadae hazikuwamo tena baada ya kupotezana.

Kwao hakina chiku bado kulikuwa na songombingo la yahaya kutaka maamuzi ya wazee wa kaya ya mmpendekeze yeye kama ndiye mtu astahiliye kupewa mirathi japo kwa mujibu wa taratibu yahaya hakuwa mtu sahihhi anae faha kupewa miliki na mali za babake chiku alitambua fika kuwa kwa njia za kawaida hatoweza kuwashawishi wazee wale kukubaliana na mawazo yake pale itakapo wadia siku ya kuanua matanga,ikiwa ni jioni tulivu yenye upepo mwanana huku mida ikiwa inazidi yoyoma kuutafuta kigiza cha usiku aliona bora aende kilingeni kumtafuta rafikiye Kudu mawazoni mwake aliweka imani kuwa kutoka kwa rafiki yake huyu hatapata mawazo safi ya kufanya aweze kufanikisha mipango yake ya kupora na kumiliki  mali za MzeeMatango