utangulizi
Hapana kwa kweli kama hali itakuwa ivi siku zote hakuna hatakaye salia katika mjii huu kila kukicha hakuna nafuu wala afadhari leo unalala na hili kesho una aamka na lile mmh,hata kama ni umaskini hapa umezidi ama kuna anae tuchawi kwani hali hii sio bure Sada alikuwa akilalama mwenyewe pasipo kujua kuwa sauti yake ilisikika kwa Kapemba
Kapemba; Mwenzangu vipi mbona walalama pekeako uko utokako kuna heri..?
Sada; Mmh kama kungekuwa na heri wazani ningekuwa na hali .!!!! uko hapana afadhari wala unafuu
Kapemba; mapungufu uwa hayakosekani kwa binadamu ndugu yangu la muhimu ni kukubaliana na hali ilivyo tu kisha unatafuta njia ya kujikwamua hapo ulipokwama.
Sada; ama kwani we umwenyeji wa wapi..!!
Kapemba; mbona washituka..? mie ni mzawa wa hapahapa ila sipo hapa kwa kitambo kidogo
Sada; kumbe basi we ni wakuja na shida zetu sisi hapa bado ujazitambua vyema ukikutana na watu kenda kama mimi nadhani utapata ufahamu japo kwa uchache na hauta shangaa tena kuona binti mdogo kama mie nikiwa katika hali ngumu kiasi cha kuchanganya kichwa change ivi.
Kapemba; samahani najua kila mtu anamahitaji na kupitia uhitaji wake hapo ndo changamoto zinapoanzia sasa mwenzangu naomba kwanza kufahamie kabla ya kufika mbali katika mazungumzo yetu mimi naitwa kapemba binti wa watatu wa Mzee Nsindano sijui waitwa nani?
Sada; eeh we ni binti wa Mzee Nsindano wa pale kwenye bonde la udongo mzuri Ndio hapohapo wala ujakosea {sauti ya Kapemba ilidakia} mwee kweli dunia duara na maisha yanabadilika kwakweli umekuwa rafiki yangu yaani kama vile babako alivyopataga bahati yakupata ardhi nzuri imekuiwa vivyo ivyo hadi na kwako Mmmh unasema nimebadilika kwani we nani na kilichobadilika ni kipi? {Kapemba alioji kwa sauti ya mshang`ao} ona sasa yani mpaka muda huu bado ujatambua waongea na nani sada alisema kwa kusononeka kisha akaendelea huko mjini sijui walikuwa wanakupa chakula gani ? kimekusahaulisha kila kitu cha huku mimi ni malkia wa undazi.
Kapemba; aaahaaah jamani Sada Madoso masiku mengi yamepita rafiki yangu na mbona umekuwa ivi kulikoni tena pacha wangu maisha tu yamenichagua mwenzangu hakuna kingine {alidakia sada kwa sauti ya kinyonge iliyojawa simanzi} kapemba aliendelea Ebu nambie bhana kuna nini kimefanya uwe katika hali hii maana hata kama ni maisha kwa stahili hii uliyonayo hapana mwenzangu mtazamo wangu uwaga nyinyi saivi mtakuwa wafanyabiashara mashuhuri wa mazao ya hapa kijiji..
Sada; nadhani bado tupo pamoja nitakwambia tu na utaitambua hali halisi ya maisha yangu naya vijana wengine wa hapa kijiji nikianza kusema saiv haitakuwa vyema na waweza usielewe lolote kwani mabo haypo vile ufikiliavyo vijana wote wakipindi kile uwajuao hawapo tena
Sada alishindwa kujizuia nakuanza kulia kapemba alimsogeleana nakukumbatiana uku wote sura zao zikiwa na majonzi na macho yakiwa yanatirikwa na machozi ya simanzi yenye mchanganyiko wa furaha ya kukutana tena baada yakupotezana kwa kitambo kirefu ilikuwa yapata miaka takribani ishirini tangu kupotezana kwao taswira zao za utoto hazikuwa zikionekana tena na wala zile fikra zao za kitoto juu ya maisha yao ya baadae hazikuwamo tena baada ya kupotezana.
Kwao hakina chiku bado kulikuwa na songombingo la yahaya kutaka maamuzi ya wazee wa kaya ya mmpendekeze yeye kama ndiye mtu astahiliye kupewa mirathi japo kwa mujibu wa taratibu yahaya hakuwa mtu sahihhi anae faha kupewa miliki na mali za babake chiku alitambua fika kuwa kwa njia za kawaida hatoweza kuwashawishi wazee wale kukubaliana na mawazo yake pale itakapo wadia siku ya kuanua matanga,ikiwa ni jioni tulivu yenye upepo mwanana huku mida ikiwa inazidi yoyoma kuutafuta kigiza cha usiku aliona bora aende kilingeni kumtafuta rafikiye Kudu mawazoni mwake aliweka imani kuwa kutoka kwa rafiki yake huyu hatapata mawazo safi ya kufanya aweze kufanikisha mipango yake ya kupora na kumiliki mali za MzeeMatango
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni