Jumanne, 6 Septemba 2016

TAMU NA CHUNGU

sehemu ya tatu



Yahaya; Ndugu yangu najua wajua fika kuwa wiki kadhaa tu koo yangu ilipatwa na tatizo na kuondokewa na mmoja wa ndugu muhimu sana ndio nalijua hilo si kuhusu kufariki kwa Bwana Matango {kudu alidakia} haswa sasa na ndhani wakumbuka kuwa adhima yangu ni kuwa na mimliki kubwa na nzuri na pahala pa kufanikisha hili ni katika kushika milki ya huyu ndugu yangu na swala hili litatukia baada ya wiki ya pili ya msiba kwisha yaani siku ya kuanua matanga wote tutakapokuwa  kwenye kikao cha wazee wa koo shida ni kwamba taratibu za koo hazinipi ruhusa ya kushika mali hizi rafiki yangu naomba busara zako kwani kichwa changu kina chemka.
Kudu;mhh sasa hapo mie sidhani kama nitakuwa na uwezo wakufanza lolote maana kuna mambo ambayo unataka kuchanganya na mwisho wake uwaga sio mzuri  kakangu
Yahaya; kwanini ushindwe na mambo gani hayo  unayoyaongelea wewe?


Kudu;Unajua vitu tunavyofanya sikuzote uwa ni mabaya ila kwakuwa tunafanya kwa maslai binafsi uwa tunafanya kuwa halali ila katika swala hili na maelezo yako hayo hapo kuna busara za wazee na tambua fika maamuzi yao uwa hayapingwi kwakuwa wanatumia hekima zao pili kuna mila na desturi katika jambo hili hata kama nitakupa mashauri ukumbuke hii miiko iliyopo kwenye jamii yetu haswa katika jambo hili ulilokujanalo.
Yahaya;Sawa hayo yote nayatambua vyema lakini namie nina matamanio yangu na ndio sababu ya kukutafuta na kukuleta mpaka pahali hapa nakutambua vyema bwanaKudu na nina imani kuwa hata wewe wanitambua vilivyo na hali zangu wazijua  fika sina hakika kuwa utaniona lofa au kuniweka katika kundi la wapuuzi kwa maamuzi haya niliyonayo
Kudu;kwasasa saivi ndo naelewa adhima yako vilivyo na naomba ukumbuke mambo mawili yale niliyosema ukisha kubaliana nayo hapo nami nitakuwa na nafasi ya kueleza maono yangu ili tusiweze kulumbana sana nakubaliana nayo {ilikuwa sauti ya kinyonge toka kwa Yahaya} hapo sawa sasa jambo la kwanza ilikuweza kushawishi hisia na busara za wazee pamoja na mamaChiku mwenyewe badili msimamo wako uwe chanya kwa watu wote hawa
kohkohhkohoKudu alitoa kikohozi cha kusafisha koo lake iliaweze kusikika vyema kisha akaendelea kama utafanya shingo yako kuwa ngumu katika hili tambua fika mawazo ya wazee yatakuwa kinyume na wewe na tena katika mila na desturi za hapa linapotokea swala kama hili wazee wanaangalia hali ya familia husika na kama mama wa familia anajiweza wao umpatia jukumu la kutafuta mtu wa kumrithi na kummilikisha mali zote binafsi yangu naona hii ni nafasi pekee ya kumshawishi mamachiku kukubaliana na matakwa japo sio kwaku mueleza yale utakayo laa ila jaribu kuteka ule ukaribu wako kwake sijui kama tu pamoja.
Yahaya;mmmh mh haya maji ya shingo ila hakuna tatizo ngoja nitaona itakavyokuwa kabla ya siku kufika
Maono ya yahaya sasa yalikuwa yakiwaza utajili wa mali kedekede na kupewa mtu wa kupokea kauli na maagizo yake bila kuhoji nini cha ziada moyoni mwake hakuwa na lepe la huruma kwa familia hii iliyojawa majonzi
Kudu;ndugu yangu swala lolote linanalo hitaji mikono na busara za wazee uwa sio jambo jepesi lakini nadhani itafaa kama ukimrithi na mfiwa mwenyewe
Yahaya;mmh eeenh hapo hapa tena ilo swala hata silitaki kabisaa…yani pale mie nataka mali tu maisha ya chiku na mamaye sitaki yawe yangu hata punje.
Kudu;basi hapo ndo unapokosea ila hakuna namna na mie mpaka sasa sina la kuongeza kama kila neno unaona mzigo hapo namie na nanawa mikono kaka tusubiri maamuzi ya balaza la wazee hatuna uwezo wa kuingilia watakachotaka kufanya.
Yahaya;mwee sawa rafiki yangu katika hili nimeingia mkenge ila katika ukoo wote mie ndo mkubwa na hili swala hakika litakuja kwangu tu.
Kudu;sawa tusubiri ….. af wakati unatuacha ebu tuanze kurejea
Wakati haukuwa rafiki kwao ilibidi wanyanyuke nakuanza kujerea majengo Yahaya hakuamini kama swala hili limekuwa gumu kiasi kwamba hata kudu alikuwa na nafsi ya uwoga kutoa na kueleza mashauri yake juu ya namna ya kulifanikisha na njia nzima bado alikuwa akiona giza kubwa kwani hakuona hatma ya kile alichokuwa akitaka kupata.

Akiwa katika chumba chake Kapemba bado alikuwa na taswira nzito kwa kujaribu kutengeneza picha ya namna ambavyo kijana wa umri wake anavyokutana na changamoto nzito na kukosa msaada wa kuzitatua,alijaribu kufikiria hali ya maisha katika kijiji chao ilivyokuwa hapo awali na kulinganisha na hali aliyoipata katika sauti ya Sada katika siku ile marazote alipotaka kupata usingizi sauti na sura ya huzuni iliyokata tamaa ya rafikiye kipenzi sada ilijitokeza na kufanya usingizi kuwa wenye maruweruwe mengi hapana nitasema na Baba kesho labda atakuwa anajua chanzo {alijisemea Kapemba na kulazimisha kujilaza}


Usikose kufuatiali sehemu ijayo..............



Jumatano, 31 Agosti 2016

TAMU NA CHUNGU


sehemu ya pili



Kwao hakina chiku bado kulikuwa na songombingo la yahaya kutaka maamuzi ya wazee wa kaya ya mmpendekeze yeye kama ndiye mtu astahiliye kupewa mirathi japo kwa mujibu wa taratibu yahaya hakuwa mtu sahihhi anae faha kupewa miliki na mali za babake chiku alitambua fika kuwa kwa njia za kawaida hatoweza kuwashawishi wazee wale kukubaliana na mawazo yake pale itakapo wadia siku ya kuanua matanga,ikiwa ni jioni tulivu yenye upepo mwanana huku mida ikiwa inazidi yoyoma kuutafuta kigiza cha usiku aliona bora aende kilingeni kumtafuta rafikiye Kudu mawazoni mwake aliweka imani kuwa kutoka kwa rafiki yake huyu hatapata mawazo safi ya kufanya aweze kufanikisha mipango yake ya kupora na kumiliki  mali za MzeeMatango nyakati zote hawapo katika shuruba kudu ndiye aliyekuwa kimbilio lake na nyakati zote uwa asitikusilikiza mashauri anayopewa na rafikiye huyu moyoni mwake yahaya hakuwa hata na chembe ya huruma kwa hali watakayo kuwanayo wakina chiku pamoja na mamaye alichojali yeye ni kupewa miliki na kuzitumia mali hizi kwa namna itakayo konga nafsi yake vilivyo aliwaza anasa kuliko maisha ya upweke yatakayo anza kwa mama chiku na bintiye.

baada ya kufika kilingine alianza kupepesa macho kutafuta pahala alipoketi kudu 

ilichukua kama dakika mbili tu taswira ya kudu ilikuwa tayari katika mboni za macho yake mazoea ya kuwa wote kilingine yalimfanya yahaya asipate tabu sana kuzungusha mijicho yake ili kumpata rafikiye maana kudu alipendelea kukaa katika kona ya kati kalibu kabisa na kitijoto cha mamamuuza.

Nyakati zilikuwa zimesonga tangu alipoanza mwendo kwenda kilingeni jioni sasa nayo iliyoyoma na nuru ya jua ilianza kupoteza mwanagaza wake sababu ya usiri mzito wa mambo waliyotaka kuzungumza yahaya hakuona kama itakuwa busara kwa wao kuketi na kuendesha mazungumzo yao katika kilinge ila hakuwa na nguvu ya ushawishi kumuondosha kudu katika mazingira yale.

Yahaya; Habari ndugu yangu ,,,? Naona upo hapa kupumzisha akili kama ilivyo ada.
Kudu; aaahnahaha yahaya kijogoo cha mji mtu mwenye adhi yake ,, karibia sana kakamkubwa hapa si tupo tunaondoa mikosi na laana za wazee wa ardhi hii ya imarakaseko.
Yahaya; nakuona tu hapa maana upo na mashamshamu leo vipi mbona wale warembo wa pembeni hawapo pamoja nawe kunani? Umeanza yale mambo ya ajabu nisiyopenda (Kudu alilalama) basi tuachane na haya ndugu yangu mguu huu niwako nimekuja kukungata sikio ilikupata busara zako yahaya alisita kidogo
Kudu; endelea nakusikiliza mbona upo kimya tena ….! kama ni jambo la usiri sana tufanye kuzungumza baadae tukitoka hapa  au we wasemaje ?
Yahaya; rafiki yangu kama nilivyosema huu mguu ni wako na hapa sikuja kwa adhima nyingine yoyote ile zaidi ya kutaka kuonana nawe kuzungumza jambo hili basi,maana ili jambo lina ninyima raha na Amani ya kufanya mambo mengine hata kama nitajilazimisha vipi bado nakuwa sina uhuru kama awali napolifikiria swala hili sasa naomba tutoke hapa twende nje kidogo naitaji busara zako, mmmh kweli ili jambo la hatati sana mtu mzima mwenzangu mpaka umekuwa na hali ama kweli muungwana akivuliwa nguo sharti achutame haya twende huku njee {kudu alikubaliana na mawazo ya yahaya kisha wote wakanyanyuka na kuanza kwenda nje ya kilinge}
Kudu; haya mkubwa mwenzangu ebu ni habarishe kuhusu ilo swala maana ushaanza kutia ofu namie hapa naona nafsi inajawa mashaka Je kunani huku au lile sekeseke la wale wafugaji kutoka katika ardhi ya udongo mzuri limekuja tena?
Yahaya; hapana sio jambo hili walasindani kama lile swala la weza kurudi tena hili la leo ni jipya tena jipya haswa, skiliza ebu twende hapo kwenye mawe ya mtemi tukaketi hatuwezi kuongelea hili jambo hapa rafiki yangu
Kudu hakuwa na kinyonge wala hakutaka kubishabisha sana juu ya maombi ya yahaya japokuwa alitambua fika kuwa tayari raha zake zimekwisha katishwa na hatapata nafasi tena ya kuzirudia kwa wakati ule maana tayari nyakati zake zilikuwa zimekwisha muacha alifuatana na rafikiye mpaka katika sehemu ya mawe ya mtemi
Kudu; bwanamkubwa haya sasa tumefika ebu keti na unihabarishe juu ya hayo maswala yako nakuona hauko sawa na nadhani hata moyo wako pia una shuruba sawa na hali ya macho yako nipo hapa sema nami
Yahaya; Ndugu yangu najua wajua fika kuwa wiki kadhaa tu koo yangu ilipatwa na tatizo na kuondokewa na mmoja wa ndugu muhimu sana ndio nalijua hilo si kuhusu kufariki kwa Bwana Matango {kudu alidakia} haswa sasa na ndhani wakumbuka kuwa adhima yangu ni kuwa na mimliki kubwa na nzuri na pahala pa kufanikisha hili ni katika kushika milki ya huyu ndugu yangu na swala hili litatukia baada ya wiki ya pili ya msiba kwisha yaani siku ya kuanua matanga wote tutakapokuwa  kwenye kikao cha wazee wa koo shida ni kwamba taratibu za koo hazinipi ruhusa ya kushika mali hizi rafiki yangu naomba busara zako kwani kichwa change kina chemka.
Kudu;mhh sasa hapo mie sidhani kama nitakuwa na uwezo wakufanza lolote maana kuna mambo ambayo unataka kuchanganya na mwisho wake uwaga sio mzuri  kakangu
Yahaya; kwanini ushindwe na mambo gani hayo  unayoyaongelea wewe?

Usikose kufuatilia sehemu ijayo.

Jumamosi, 27 Agosti 2016

TAMU NA CHUNGU

utangulizi



Hapana kwa kweli kama hali itakuwa ivi siku zote hakuna hatakaye salia katika mjii huu kila kukicha hakuna nafuu wala afadhari leo unalala na hili kesho una aamka na lile mmh,hata kama ni umaskini hapa umezidi ama kuna anae tuchawi kwani hali hii sio bure Sada alikuwa akilalama mwenyewe pasipo kujua kuwa sauti yake ilisikika kwa Kapemba
Kapemba; Mwenzangu vipi mbona walalama pekeako uko utokako kuna heri..?
Sada; Mmh kama kungekuwa na heri wazani ningekuwa na hali .!!!! uko hapana afadhari wala unafuu
Kapemba; mapungufu uwa hayakosekani kwa binadamu ndugu yangu la muhimu ni kukubaliana na hali ilivyo tu kisha unatafuta njia ya kujikwamua hapo ulipokwama.
Sada; ama kwani we umwenyeji wa wapi..!!
Kapemba; mbona washituka..? mie ni mzawa wa hapahapa ila sipo hapa kwa kitambo kidogo
Sada; kumbe basi we ni wakuja na shida zetu sisi hapa bado ujazitambua vyema ukikutana na watu  kenda kama mimi nadhani utapata ufahamu japo kwa uchache na hauta shangaa tena kuona binti mdogo kama mie nikiwa katika hali ngumu kiasi cha kuchanganya kichwa change ivi.
Kapemba; samahani najua kila mtu anamahitaji na kupitia uhitaji wake hapo ndo changamoto zinapoanzia sasa mwenzangu naomba kwanza kufahamie kabla ya kufika mbali katika mazungumzo yetu mimi naitwa kapemba binti wa watatu wa Mzee Nsindano sijui waitwa nani?
Sada; eeh we ni binti wa Mzee Nsindano wa pale kwenye bonde la udongo mzuri Ndio hapohapo wala ujakosea {sauti ya Kapemba ilidakia} mwee kweli dunia duara na maisha yanabadilika kwakweli umekuwa rafiki yangu yaani kama vile babako alivyopataga bahati yakupata ardhi nzuri imekuiwa vivyo ivyo hadi na kwako Mmmh unasema nimebadilika kwani we nani na kilichobadilika ni kipi? {Kapemba alioji kwa sauti ya mshang`ao} ona sasa yani mpaka muda huu bado ujatambua waongea na nani sada alisema kwa kusononeka kisha akaendelea huko mjini sijui walikuwa wanakupa chakula gani ? kimekusahaulisha kila kitu cha huku  mimi ni malkia wa undazi.
Kapemba; aaahaaah jamani Sada Madoso masiku mengi yamepita rafiki yangu na mbona umekuwa ivi kulikoni tena pacha wangu maisha tu yamenichagua mwenzangu hakuna kingine {alidakia sada kwa sauti ya kinyonge iliyojawa simanzi} kapemba aliendelea Ebu nambie bhana kuna nini kimefanya uwe katika hali hii maana hata kama ni maisha kwa stahili hii uliyonayo hapana mwenzangu mtazamo wangu uwaga nyinyi saivi mtakuwa wafanyabiashara mashuhuri wa mazao ya hapa kijiji..
Sada; nadhani bado tupo pamoja nitakwambia tu na utaitambua hali halisi ya maisha yangu naya vijana wengine wa hapa kijiji nikianza kusema saiv haitakuwa vyema na waweza usielewe lolote kwani mabo haypo vile ufikiliavyo vijana wote wakipindi kile uwajuao hawapo tena
Sada alishindwa kujizuia nakuanza kulia kapemba alimsogeleana nakukumbatiana uku wote sura zao zikiwa na majonzi na macho yakiwa yanatirikwa na machozi ya simanzi yenye mchanganyiko wa furaha ya kukutana tena baada yakupotezana kwa kitambo kirefu ilikuwa yapata miaka takribani ishirini tangu kupotezana kwao taswira zao za utoto hazikuwa  zikionekana tena na wala zile fikra zao za kitoto juu ya maisha yao ya baadae hazikuwamo tena baada ya kupotezana.

Kwao hakina chiku bado kulikuwa na songombingo la yahaya kutaka maamuzi ya wazee wa kaya ya mmpendekeze yeye kama ndiye mtu astahiliye kupewa mirathi japo kwa mujibu wa taratibu yahaya hakuwa mtu sahihhi anae faha kupewa miliki na mali za babake chiku alitambua fika kuwa kwa njia za kawaida hatoweza kuwashawishi wazee wale kukubaliana na mawazo yake pale itakapo wadia siku ya kuanua matanga,ikiwa ni jioni tulivu yenye upepo mwanana huku mida ikiwa inazidi yoyoma kuutafuta kigiza cha usiku aliona bora aende kilingeni kumtafuta rafikiye Kudu mawazoni mwake aliweka imani kuwa kutoka kwa rafiki yake huyu hatapata mawazo safi ya kufanya aweze kufanikisha mipango yake ya kupora na kumiliki  mali za MzeeMatango 

Jumapili, 3 Januari 2016

SIKITIKO LANGU (siku uumbiwa shida)






Mwili wake uliojengeka kikamilifu,kifua kipana na urefu wake uliosindikizwa na ngozi ya maji ya kunde vilimshawishi kila binti kukiri kwamba Eze kado alikuwa mtu wa shughuli pevu kitandani,"Umbo langu halijengwi na mpira wa miguu wala gym" alipenda kujitapa Eze kila anaposifiwa kwamba "He is gentleman" ni ukweli mtupu wala alikuwa hajisifii hata kiduchu Japo maisha yake yalikuwa ya kawaida sana hakuwa na makuu ila sifa zake zili enea zaidi kutokana na maneno ya majirani zake hasa wasichana walikwisha kuonja mambo yake.
Kutoka na maisha duni ya vijana wengi walio kuwa katika mtaa mmoja hasa wale waliokuwa  na urafiki pamoja na Eze waliona mambo anayofanya ni kama laana Kitendo cha mtoto wa kiume kuwa tayari kufanya mapenzi kwa ajili ya pesa lilikuwa jambo la ajabu sana kwao na sio ivo tu kwani jambo hili na vitu vilivyokuwa vinafanyika na Eze vilikuwa vitu vigeni katika macho yao japo Fikra zao na Mitazamo yao hata haikuwa na tija yoyote  kwa Eze yeye aliona swala hilo ni sawa tu tena ni ajira tosha na kama alipata nafasi ya kulitenda basi alifanya kwa juhudi zote na hii ni sababu tosha ya yeye kuweza kunasa warembo wengi tena wenye pesa zao.
Baadhi ya vijana waliokuwa na mtazamo tofauti na jinsi yeye alivyokuwa walikuwa akijitenga nae ili halikuwa tatizo kwake maana yeye Eze alikuwa mtu wa watu alipata marafiki wa kila rika kwani alikuwa mchangamfu,mcheshi na mwenye kusikia kama ataona jambo hilo kuwa zuri maisha yake yote yalikuwa ni ya kukutana na watu wapya na kufanya urafiki  kwa wale waliokuwa  wakiishi kwa wazazi wao daima hakupewa  ridha hata kidogo wazazi wao hakuwa wakipenda kuona vijana wao wakimbatana na Eze maranyingi waliwaambia wa mkwepe sana kwani wengi walikuwa na mtazamo sawa na falsafa hii UKIWA KARIBU NA UARIDI BASI NAWE UTANUKIA .
*****************************************************************************
Eze aliependa kuishi vile amabavyo akili yake ilikuwa inamtuma na hakuiona ubaya wala tatizo katika maisha ambayo yeye alikuwa ameichagua kuishi ,alipenda sana kuwa na marafiki wengi lakini kutokana na namna wengi wao walivyokuwa wanamchukulia kamwe hakuwa mtu wakisirani aliheshimu maamuzi yao na hata siku moja hakuwahi kuwa na Fikra ya kupata matatizo nje ya lile la kufumaniwa akiwa na mke wa mtu maana alijua fika mambo yatakayo mkumba siku iyo atakayo fumwa hofu iyo ilifanya akawa muoga sana kufuatilia au  kuwa karibu na wake za watu hakupenda kabisa mazoea nao.
Katika mawazo yake sio kwamba alikuwa hana tamaa kwa hawa wake za watu laa woga wake tu ndo ulifanya atafute njia ya kumuepusha yeye juu ya mabalaa yatakayo mpata pale atakapo fumwa na mke wa mtu aliweza kujikinga kiasi chake na akili mwake alikuwa na kauli moja tu ya kumlinda  katika  swala hili kwamba MKE WA MTU NI SUMU.
Eze alikuwa mtu wa totoz  kila wiki aliweza kubadili hata mara tatu,si yeye aliyewatongoza mara nyingi wengne walitaka huduma wenyewe hata bila ya yeye kutamka Neno "NAKUPENDA"kati yao,mh! sijui walikuwa wanapata nini lakin kamwe hawakuisha wala kukatika katka ghetto la Eze hakuwa na kazi maalum lakin kutokana na kujibanabana kwake aliweza kupanga chumba katika nyumba ya Mzeejobu mahali ambapo palikuwa kipozeo cha walimbende wengi na walikuwa wana kuja na visingizio vingi vingi tu mara watake chaja ya simu,wengine walikuwa wanakuja kulizia muda katika ghetto lake hakuwa na mambo mengi sana ,maana lilikuwa ni ghetto la kisela zaid yeye alikuwa na kitanda ,redio,kijimeza kidogo kilichokuwa na kopo la kuwekea mswaki/dawa na vitu vingne vidogovidogo tu  ila ukifika muda wao tu wenyewe walikuwa wanakuja ili mladi tu kumuona au kusikia sauti yake.
Kitanda chake ni rafiki zake pekee waliokiita sita kwa sita lakin kila binti aliyebahatika kulala
chali au walau mikono tu ndo kushika kitandani wakat miguu iko chini walitoka na majina yao
tofauti,wengne walisema 'konani ' wengne 'darajani' na wengi wao walipaita "MACHINJIONI" jina la MACHINJIONI hili ndo lilikuwa maarufu sana kwa wote waliokuwa wanaishi na Eze katika nyumba ile haswa wale waliojua tabia yake wengi walikifanisha  chumba chake na #Boma yaani (sehemu ya kuogeshea mifugo kila ngo'mbe,mbuzi,kondoo wa kila aina  lazima azamie kwenye maji yake haijalishi mnyama huyu atakuwa na afya njema au mgonjwa) ni lazima hataoshwa tu, ivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Eze kamwe hakuchangua msichana wakulala nae awe mweusi ,mweupe ,mnene,mwembamba au MSICHANA mwenye sifa yoyote aliochozingatia yeye ni uzima wa afya zao tu japo hakuwa tayari hata siku moja kwenda kujipima gonjwa lolote la zinaa.
Maisha haya kwake Eze yalikuwa mazuri tu na alifurahia sana kwa namna moja yaliweza kuraisisha ugumu katika swala la uchumi kwani  katika siku zote yeye hakuwa mtu wa presha kwamba sina hela ,chakula au mavazi kwani baadhi ya wasichana wengi aliokuwa nao walikuwa wakijiweza kiuchumi na pale walipo kuwa wamefuraishwa au kukunwa ile inavyopaswa  waliweza kukunjua  pochi zao kwa rohosafi kabisa na kumkabizi kiasi kidogo cha pesa cha kusaidia katika mahitaji yake pale.
Eze hakuwa na kumbukumbu ya kulalamikiwa na msichana eti kuwa hajaridhika hata kama siku iyo alikuwa na uchovu kasi gani yeye alifanya kila njia kuweza kufuraisha moyo wa binti yoyote atakaye kuwa nae kwa wakati huo badala yake weng walimwambia "Eze unaniua" wakati kiuno bado wanazungusha.ah! mapenzi bwana mambo haya yalikuwa yakimfuraisha sana Eze na alikuwa najiona kidume haswa
Kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi wa wapangaji ambayo alikuwa anaishi nao katika nyumba ya Mzee jobu alilazimika kuhama na kwenda katika mtaa wa mbali kidogo  na hapo alipokuwa akiishi mwanzo sababu kubwa ya kufanya yeye kuondoka ni baada mmoja wa wapangaji wenzake aitwae baba sukudhan kuhisi kuwa Eze anatembea na mkewe kwa woga alikuwa nao Eze hakupenda mambo kuwa makubwa sana na njia peke akaona ni bora kuondoka tu mahala pale kwani tabia yake ilikuwa nongwa kwa wapangaji wenzake hasa wale wote waliokuwa na wake zao.

Pamoja na kuponapona toka katika lawama na mtego wa babasikudhan hakuwa mwisho wa tabia ya Eze japo swala hili lilikuwa nyenzo tosha ya kumfanya yeye kuwa makini zaidi kwa ugeni wake pale mtaani wengi hawakuwa na mazoea na tabia yake japo walikuwa wanajua sifa zake chache tu .

Jumatatu, 7 Desemba 2015

SAFARI YA ISOKE

Hapo ndo nilipokuwa na CHOCHEA hasira zao zaidi mpaka Ulifika wakati baba na mama walitaka kuniachia laana na hapo ndo nika kumbuka pia maneno ya sharon na angnes baada ya kuwadanganya wazazi wangu zaidi ya miaka kumi toka nipate pesa na kuwajengea nyumba.


Japo maneno ya kina agnes na sharon  yalikuwa magumu kueleweka kwangu kulikuwa  na msingi kidogo kwa waliyosema na hawa ndo kidogo nilikuwa naona kama wananiwazia mema ila sio kwa 100% sababu wote hawa walikuwa wanakaa kwenye vikao vya kunisema pale ofisini Agnes alinambia kaka maisha ni safari ndefu ila usikate tamaa mie pia nilipitia uko uko kwan wazazi wangu walikataa mtu niliye mpenda kwa dhati na nilikuwa tayar kumvumilia kwa kila hali
lakini......chokochoko za ndugu zake na maisha waliyoleta hapo ilikuwa bala Sauti ya sharon pia ikanijia boss wangu Pole ila haya ni mapito tu ujakosea sana maana sisi wanawake tuna vimbwanga vingi sana leo utaniona nmetulia kesho ukinipa nachotaka tu tena kwenye kiapo ndoa wewe tena basi si unaona kila siku watu wanavyo lia umo majumbani ILA ANGALIA UZEE UO UNAKUJA kakangu.

Nilizid kukosa amani zaid ya ilivyokuwa awali maana maneno ya #Mzee yalikuwa tishio zaid
Na kilicho kuwa kina ni vuruga kabisaaaaaaaaaaaaa na kunitoa katika mstari wa AMANI ni icho kisa cha jamaa yangu kadinko Baada ya kupata kizunguzungu kwa kufikiria nini itakuwa hatma ya hili swala langu mawazo yali rudi upya tena kwenye mkasa wa kadinko ambao huu pekee ndo ulikuwa tishio katika swala langu la kutafuta, kupata na kukuamini #mwanamke yoyote kuwa mke wangu
Nakumbuka siku izo nili toka tu katika shughuli za ofisini na kwa bahati nzuri nilikutana na evad kwa utani tu nikamuliza ivi hayo una andika yamekupata wewe nini? Au kuna ndugu yako yasha mkutaaa?? akanambia hapana bhna haya maisha tu yana mambo mengi na hayo ndo ya nafanya akili iende mbali ivo DAH ila kweli sasa acha mie niende kwa jamaa angu Kandiko

Jumatano, 11 Novemba 2015

SAFARI YA ISOKE

Watu wengi walio ni ona walinishangaa sana, kwani sikuwahi kuonekana na mwanamke yoyote katika ukarbu ule wa kuhisiwa kuwa nina #uhusiano au niliyeongozana naye katika maisha yangu nakumwita mchumba . Si kwamba nilikuwa na hitilafu yoyote mwilini japo mawazo ya wengne hasa wasichana na wanawake niliokuwa nafanya nao kazi pale ofisini yalinipa ofu baada ya kumsikia  msaidizi wangu wa kike(secretary) alipokuwa anateta na wenzake kuwa #jogooWanguHapandiMtungi kwa kipindi chote cha kazi sikuwahi kumuonyesha ishara yoyote ya kumtaka na kilicho ni kera zaid ni kusikia toka kwa wanaume waliokuwa chini yangu kuwa #mtotomimiSirdhki na wazazi wangu wamepata hasara.Hapana nilikuwa mwanaume rijali, na sikupenda kujihusisha na ngono,kwani magonjwa yamezagaa kama inzi kwenye mzoga.


Licha ya magonjwa, ni dhambi kubwa kuzini nje ya ndoa. Nilitambua kwamba jambo hilo halimfurahishi muumba hata kidogo.Siku zote nilikuwa nikijilaumu,ikafikia wakati nikitaka kuokota mwanamke hata baa,lakini nika kumbuka kisa cha jamaa mmoja anaitwa kadinko ila ye anapenda kujiita kado wakat yeye anatafuta mtu wa kuishi nae alipata tabu na kupitia kipind kigumu kama mimi, ila yeye alikuwa na haraka kidogo hali iliyo fanya akagombana mpaka na dadake violeth miez mitatu kabla ya ndoa  kufika na kwan dadake akukubaliana na swala la kuolewa kwa uyo bint ambae bwana Kandiko ali mchagua na kuona kuwa anafaa kwani hakutaka kabisa kusubr kwa kipind chote bila kuwa na uyo bint kama mwenzi wake.


kwani imani yake ili kuwa na msukumo kuwa tabia za wana ndoa ujengeka nakuwa safi baada ya kuwa pamoja akasahau kabisa sio tu maneno aliyo ambiwa na dadake bali ali sahau hata maneno ya #wahenga kuwa #MkemwenyetabianjemaniNgaokwamumewe Aliyakumbuka maneno haya baada ya mambo yake kumwendea mlama wiki moja kabla ya  #shereheyaHARUSI yake kufanyika Kilinitisha Sana kisa cha kuvunjika kwa harusi ya kadinko kabla hata sijaweka wazi juu ya mkasa uo kuna kosa ambalo wazazi wengi wana fanya na kwao uona ni vyema tu, Yaani binafsi yangu Nilihitaji kuwa na subira nikihisi pengine ningempata atakaye nipenda na mimi kupenda.

Umri wangu ulisogea kufikia miaka arobaini. Hali ambayo iliwaogopesha sana wazazi wangu,waliokuwa wazee wa kujikongoja.  Nilizaliwa mtoto pekee wa kiume na dada zangu watatu.Wazazi wangu walichoka na maneno yangu.“Bado umri wa kuona. Nitaoa Mungu akipenda,mke mwema hupewa na Mungu” Miaka yote huwa nilikuwa najitetea hivyo .
Hapo ndo nilipokuwa na CHOCHEA hasira zao zaidi mpaka Ulifika wakati baba na mama walitaka kuniachia laana na hapo ndo nika kumbuka pia maneno ya sharon na angnes baada ya kuwadanganya wazazi wangu zaidi ya miaka kumi toka nipate pesa na kuwajengea nyumba.

itaendele

Jumanne, 1 Septemba 2015

SAFARI YA ISOKE





Kutokana na naswali la rafiki yangu katalambuga kuwa Nilishindwa kuokota mke ilimradi mke kama vile mtu anavyookota nyanya sokoni na kulipa pesa, nafikiri hata anayeokota nyanya nae huchagua.


Japo kuna usemi usemao mchagua nazi hupata koroma usemi huo niliupinga na kuutupilia mbali.
Niliamini usemi wa kuoa ni kuoa pengine ningefanya hivyo basi ndoa yangu isinge kuwa na
ladha ya unyumba na isingedumu maishani.

Nilijawa na imani kuwa mke mwema hupewa na Mungu, niliishi kwa matumaini ya Mungu na nilitegemea msaada mkubwa kutoka kwake mpaka kipindi hiki Mungu aliwapa Wazazi wangu baraka walikuwa hai wakinisubiri nioe wamuone mkwe na wajukuu wao kabla ya wakat wao wa kufariki kuwa fikia japo Kwa bahati mbaya siku weza kupewa upeo wa kuona mchumba mwema mapema yote hii ambaye angekuwa mke wangu,

japo nilikuwa na kazi nzuri na nafasi yangu kazini ili nifanya nionekane maridadi saa zote.
Watu wengi walio ni ona walinishangaa sana,

itaendelea